The chat will start when you send the first message.
1Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.[#Efe 4:22; Yak 1:21]
2Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;[#1 Kor 3:2; Ebr 5:12,13; Mt 18:3]
3ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.[#Zab 34:8]
4Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.[#Zab 118:22; Isa 28:16; Mt 21:42; Mdo 4:11]
5Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.[#Efe 2:21,22; Rum 12:1]
6Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko[#Isa 28:16; Rum 9:33]
Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima,
Na kila amwaminiye hatatahayarika.
7Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,[#Zab 118:22; Mt 21:42]
Jiwe walilolikataa waashi,
Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
8Tena,[#Isa 8:14-15; Rum 9:33]
Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha.
Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.
9Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;[#Kut 19:5-6; Isa 43:20-21; Kum 4:20; 7:6; 14:2; Tit 2:14; Isa 9:2; Mdo 26:18; 2 Kor 4:6; Efe 5:8; Flp 2:15; Ufu 1:6]
10ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.[#Hos 1:6,9; 2:1,23; Rum 9:25]
11Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.[#Zab 39:12; Gal 5:17,24; Efe 2:19; Yak 4:1]
12Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.[#Isa 10:3; Mt 5:16; Yak 3:13]
13Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa;[#Rum 13:1-7; Tit 3:1]
14ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema.
15Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;[#1 Pet 3:16]
16kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu.[#Gal 5:13]
17Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.[#Rum 12:10; Mit 24:21; Mt 22:21]
18Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa hofu nyingi, sio wao walio wema na wenye upole tu, bali nao walio wakali.[#Efe 6:5; Tit 2:9]
19Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki.
20Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.[#1 Pet 3:14,17; 4:13,14; Mt 5:10]
21Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.[#Mt 16:24; Yn 13:15]
22Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.[#Isa 53:9; Yn 8:46; 2 Kor 5:21]
23Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.[#Isa 53:7]
24Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.[#Isa 53:5,12; 1 Yoh 3:5; Rum 6:11; Ebr 9:28]
25Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.[#Isa 53:6; Eze 34:5; 1 Pet 5:4; Yn 10:12]