1 The 1

1 The 1

Salamu

1Paulo, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba, na katika Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani.[#Mdo 17:1; 15:40; 2 The 1:1]

Imani na Kielelezo cha Wathesalonike

2Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu.[#2 The 1:11]

3Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu.[#1 Kor 13:13; Kol 1:4,5]

4Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu;

5ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.[#1 Kor 2:5]

6Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu.[#Mdo 17:5-9; 13:52; 1 Kor 4:16; 2 The 3:9]

7Hata mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya.[#1 The 4:10; Flp 3:7; 1 Pet 5:3]

8Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote.[#Rum 1:8]

9Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli;[#Mdo 14:15; Yn 17:3; 1 Kor 12:2]

10na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.[#1 The 5:9; Tit 2:13; Mdo 17:31]

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania