The chat will start when you send the first message.
1Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu;[#Kol 4:3; 1 The 5:25]
2tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.
3Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.[#1 The 5:24]
4Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza, tena kwamba mtayafanya.[#1 The 4:10; Gal 5:10; 2 Kor 7:16]
5Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.
6Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.[#Mt 18:17; Rum 16:17; 1 The 5:14; 4:1]
7Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata; kwa sababu hatukuenda bila utaratibu kwenu;[#1 The 2:1; 1:6]
8wala hatukula chakula kwa mtu ye yote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulitenda kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote.[#1 Kor 4:12; Flp 3:17; 1 The 2:9]
9Si kwamba hatuna amri, lakini makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate.[#Mt 10:10; 1 Kor 4:16; 1 The 1:6,7]
10Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.[#Mwa 3:19; 1 The 3:4; 4:11]
11Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.[#1 The 5:14]
12Basi twawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.[#1 The 4:11]
13Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema.[#Gal 6:9]
14Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari;[#1 Kor 5:9,11]
15lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.[#1 The 5:13,14]
16Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.[#1 The 5:23]
17Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila waraka, ndio mwandiko wangu.[#1 Kor 16:21]
18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.