Kut 1

Kut 1

1Basi majina ya wana wa Israeli walioingia Misri ni haya; kila mtu pamoja na jamaa zake walikuja pamoja na Yakobo.[#Mwa 46:8-27; Kut 6:14]

2Reubeni, na Simeoni na Lawi, na Yuda;

3na Isakari, na Zabuloni, na Benyamini;

4na Dani, na Naftali, na Gadi, na Asheri.

5Na nafsi zile zote zilizotoka viunoni mwa Yakobo zilikuwa ni nafsi sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo.[#Mwa 46:26; Kum 10:22]

6Yusufu akafa, na ndugu zake wote, na watu wote wa kizazi kile.[#Mwa 50:26; Mdo 7:15; Mhu 1:4]

7Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.[#Mdo 7:17; Mwa 46:3; Kum 26:5; Zab 105:24]

Waisraeli Wateswa

8Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.[#Mdo 7:18]

9Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.[#Zab 105:24]

10Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.[#Mdo 7:19; Zab 10:2; 83:3; Ayu 5:13; Mit 28:16]

11Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.[#Mwa 15:1; Kut 2:11; 3:7; 5:4; Mit 27:3; Zab 81:6; Mwa 47:11]

12Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli.

13Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali;

14wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.[#Kut 2:23; 22:21; Law 25:14,17; Hes 20:15; Ayu 20:19; Mit 14:31; 22:22; Mdo 7:19,34; Zab 10:17,18; 81:6]

15Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua;

16akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.

17Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.[#Mit 16:6; Dan 3:16,18; 6:13; Mdo 5:29]

18Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai?

19Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia.[#Yos 2:4; 2 Sam 17:19,20]

20Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi.[#Mit 11:18; Mhu 8:12; Isa 3:10; Ebr 6:10]

21Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.[#1 Sam 2:25; 2 Sam 7:11,13,27,29; 1 Fal 2:24; 11:38; Zab 127:1]

22Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.[#Mdo 7:19]

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania