The chat will start when you send the first message.
1Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama BWANA alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe.[#Hes 20:2-13; Kut 16:1; 19:2; Hes 33:12,14]
2Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu BWANA?[#Hes 20:3; Kum 6:16; Zab 78:41; Isa 7:12; Mt 4:7; 1 Kor 10:9]
3Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung’unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu?[#Kut 16:2]
4Musa akamlilia BWANA, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe.[#1 Sam 30:6; Yn 8:59; 10:31]
5BWANA akamwambia Musa, Pita mbele ya watu, ukawachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe; na ile fimbo yako ambayo uliupiga mto kwayo, uitwae mkononi mwako, ukaende.[#Eze 2:6; Hes 20:8]
6Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli.[#Zab 105:41; 114:8; 1 Kor 10:4]
7Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba; kwa sababu ya mateto ya wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu BWANA, wakisema, Je! BWANA yu kati yetu au sivyo?[#Zab 95:8; Ebr 3:8]
8Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.[#Mwa 36:12; Hes 24:20; Kum 25:17; 1 Sam 15:2]
9Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu.[#Mdo 7:45; Ebr 4:8]
10Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima.
11Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.[#Yak 5:16]
12Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa.
13Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga.
14BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.[#Kum 25:17-19; 1 Sam 15:2-9; Kut 34:27; 1 Sam 30:1; 2 Sam 8:12; Ezr 9:14]
15Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;[#Amu 6:24; #17:15 maana yake ni BWANA ni bendera yangu.]
16akasema, BWANA ameapa; BWANA atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.