Kut 20

Kut 20

Amri Kumi za Mungu

1Mungu akanena maneno haya yote akasema,[#Kum 5:22]

2Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.[#Law 26:1; Kum 5:6; Zab 81:10; Hos 13:4; Kut 13:3]

3Usiwe na miungu mingine ila mimi.[#Kum 6:14; 2 Fal 17:35; Yer 25:6]

4Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.[#Kut 34:17; Law 19:4; 26:1; Kum 4:15-18; 27:15]

5Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,[#Kut 34:6-7; Hes 14:18; Kum 7:9-10; Yos 23:7; 24:19; 2 Fal 17:35; Isa 44:15; Nah 1:2; Isa 14:20; Yer 2:9; Eze 18:19]

6nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.[#Zab 89:34; Rum 11:28; Kum 7:9]

7Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.[#Law 19:12; Zab 15:4; Mt 5:33; Mik 6:11]

8Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.[#Kut 16:23-30; 31:12-14; Kum 5:12]

9Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;[#Kut 23:12; 31:15; 34:21; 35:2; Law 23:3; Lk 13:14]

10lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.[#Mwa 2:2; Neh 13:16]

11Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.[#Mwa 2:1-3; Kut 31:17]

12Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.[#Kum 5:16; 27:16; Yer 35:7,8; Mt 15:4; 19:19; Mk 7:10; 10:19; Lk 18:20; Efe 6:2-3; Law 19:3]

13Usiue.[#Mwa 9:6; Law 24:17; Mt 5:21; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11]

14Usizini.[#Law 20:10; Mt 5:27; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11]

15Usiibe.[#Law 19:11; 1 The 4:6; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9]

16Usimshuhudie jirani yako uongo.[#Kut 23:1; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20]

17Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.[#Rum 7:7; 13:9; Mik 2:2; Efe 5:3; Mit 6:29; Mt 5:28]

18Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali.[#Ebr 12:18-19]

19Wakamwambia Musa, Sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa.[#Gal 3:19]

20Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi.[#Mwa 22:1; Mit 3:7]

21Basi hao watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia lile giza kuu Mungu alipokuwapo.

Sheria Kuhusu Madhabahu

22BWANA akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli hivi, Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni.

23Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie.

24Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng’ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.[#2 Nya 6:6; Mwa 12:2]

25Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, hutaijenga ya mawe yaliyochongwa; kwa kuwa ukiwa wewe umetumia chombo chako katika kuichonga umeitia unajisi.[#Kum 27:5-7; Yos 8:31]

26Tena hutapanda kwenda madhabahuni kwangu kwa daraja, uchi wako usidhihirike juu yake.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania