Eze 15

Eze 15

Mzabibu Usiofaa

1Neno la BWANA likanijia, kusema,

2Mwanadamu, mzabibu una sifa gani kuliko mti mwingine, au tawi la mzabibu lililokuwa kati ya miti ya msituni?[#Zab 80:8; Hos 10:1]

3Je! Mti wake waweza kutwaliwa, ili kufanya kazi yo yote? Watu waweza kufanya chango kwa huo, ili kutundika chombo cho chote?

4Tazama, watupwa motoni kwa kuni moto umeziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea katikati, je! Wafaa kwa kazi yo yote?[#Yn 15:6]

5Tazama, ulipokuwa mzima, haukufaa kwa kazi yo yote; sembuse ukiisha kuliwa na moto, na kuteketea; je! Waweza kufaa kwa kazi yo yote?

6Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kama mzabibu kati ya miti ya msituni, niliyoupa moto uwe kuni, ndivyo nitakavyowatoa wakaao Yerusalemu.

7Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao.[#Law 17:10; Zab 34:16; Yer 21:10; 48:43,44; Isa 24:18; Amo 5:19; Eze 6:7; 7:4]

8Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, kwa sababu wamekosa, asema Bwana MUNGU.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania