The chat will start when you send the first message.
1Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,[#Ebr 4:14]
2aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.[#Hes 12:7]
3Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba.
4Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu.
5Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye;[#Hes 12:7]
6bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho.[#Efe 2:19; Kol 1:23]
7Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu,[#Zab 95:7-11]
Leo, kama mtaisikia sauti yake,
8Msifanye migumu mioyo yenu,[#Kut 17:7; Hes 20:2-5]
Kama wakati wa kukasirisha,
Siku ya kujaribiwa katika jangwa,
9Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima,
Wakaona matendo yangu miaka arobaini.
10Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki,
Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa;
Hawakuzijua njia zangu;
11Kama nilivyoapa kwa hasira yangu,[#Hes 14:21-23]
Hawataingia rahani mwangu.
12Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.
13Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.[#1 The 5:11]
14Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;[#Ebr 6:11; 11:1]
15hapo inenwapo,[#Zab 95:7-8]
Leo, kama mtaisikia sauti yake,
Msifanye migumu mioyo yenu,
Kama wakati wa kukasirisha.
16Maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa?[#Hes 14:1-35; Kut 17:1]
17Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?[#Hes 14:29; 1 Kor 10:10]
18Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi?[#Hes 14:22,23]
19Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.