Hos 12

Hos 12

1Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.[#2 Fal 17:4; Isa 30:6]

Uasi wa Muda Mrefu

2BWANA naye ana mateto na Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.

3Tumboni alimshika ndugu yake kisigino;[#Mwa 25:26; #Mwa 32:24-26]

Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu;

4Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaika[#Mwa 28:10-22]

Akashinda; alilia, na kumsihi;

Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;

5Naam, BWANA, Mungu wa majeshi;

BWANA ndilo kumbukumbu lake.

6Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.

7Ni mchuuzi, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu.

8Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wo wote uliokuwa dhambi.

9Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za karamu ya idi.[#Law 23:42-43]

10Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano.

11Je! Gileadi ni uovu? Wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng’ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.[#Amo 4:4]

12Na Yakobo alikimbia mpaka Padan-Aramu,[#Mwa 29:1-20]

Na Israeli alitumika apate mke;

Ili apate mke alichunga kondoo.

13Na kwa nabii BWANA alimtoa Israeli katika Misri,[#Kut 12:50-51]

Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.

14Efraimu amenitia hasira kali sana; kwa sababu hiyo damu yake itaachwa juu yake, na Bwana wake atamrudishia lawama yake.[#Kum 28:37; Dan 11:18]

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania