Ayu 23

Ayu 23

Ayubu Ajibu: Malalamiko yangu ni Machungu

1Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

2Hata leo mashitaka yangu yana uchungu;

Pigo langu ni zito zaidi ya kuugua kwangu.

3Laiti ningejua mahali niwezapo kumwona,

Nifike hata hapo anapokaa!

4Ningeiweka daawa yangu mbele yake,

Na kukijaza kinywa changu hoja.

5Ningeyajua maneno atakayonijibu,

Na kuelewa na hayo atakayoniambia.

6Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake?[#Ayu 9:19; Isa 27:4]

La, lakini angenisikiliza.

7Hapo walekevu wangepata kuhojiana naye;

Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele.

8Tazama, naenda mbele, wala hayuko;[#Zab 10:1; 1 Tim 6:16]

Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;

9Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona;

Hujificha upande wa kuume, hata nisimwone.

10Lakini yeye aijua njia niendeayo;[#Zab 17:3; Yak 1:12]

Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.

11Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake;[#Zab 44:18]

Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.

12Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake;

Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,

13Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza?[#Ayu 34:29; Mhu 3:14; Rum 9:19; Yak 1:17]

Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo.

14Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamuriwa;[#1 The 3:3]

Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye.

15Kwa hiyo naona taabu mbele ya uso wake;[#Zab 119:120]

Nitakapofikiri, namwogopa.

16Kwani Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia,

Naye Mwenyezi amenitaabisha;

17Maana sikufadhaishwa kwa sababu ya giza,[#Ayu 6:9]

Wala kwa sababu giza kuu limenifunika uso.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania