Ayu 34

Ayu 34

Elihu Atangaza Haki ya Mungu

1Tena Elihu akajibu na kusema,

2Sikilizeni maneno yangu, enyi wenye hekima;

Tegeni masikio kwangu, ninyi mlio na maarifa.

3Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno,

Kama vile kaakaa lionjavyo chakula.

4Na tujichagulie yaliyo ya uelekevu;

Na tujue wenyewe yaliyo mema.

5Kwani Ayubu amesema, Mimi ni mwenye haki,[#Ayu 33:9; 27:2]

Naye Mungu ameniondolea haki yangu;

6Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo;[#Ayu 9:17]

Jeraha yangu haiponyeki, nijapokuwa sina makosa.

7Je! Ni mtu gani mfano wa Ayubu,

Anywaye mzaha kama maji?

8Atembeaye na hao watendao uovu,

Na kwenda pamoja na watu wabaya.

9Kwa kuwa amenena, Haimfai mtu lo lote[#Ayu 9:22]

Kujifurahisha na Mungu.

10Kwa hiyo nisikilizeni, enyi wenye fahamu;[#Mwa 18:25; Kum 32:4]

Mungu asidhaniwe kutenda udhalimu;

Wala Mwenyezi kufanya uovu.

11Kwani atamlipa binadamu kwa kazi yake,[#Zab 62:12; Mit 24:12; Mt 16:27; Ufu 22:12]

Naye atamfanya kila mtu kuona sawasawa na njia zake

12Naam, hakika, Mungu hatatenda mabaya,

Wala Mwenyezi hatapotosha hukumu.

13Ni nani aliyemwagiza kuiangalia dunia?

Au ni nani aliyemwekea ulimwengu huu wote?

14Kama akimwekea mtu moyo wake,[#Mhu 12:7]

Akijikusanyia roho yake na pumzi zake;

15Wenye mwili wote wataangamia pamoja,

Nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi.

16Ikiwa una ufahamu, sikia neno hili;

Isikilize sauti ya maneno yangu.

17Je! Atatawala mtu aichukiaye haki hata mmoja?[#Mwa 18:25]

Nawe, je! Utamhukumia mkosa aliye na haki na mwenye nguvu?

18Je! Inafaa kumwambia mfalme, Wewe u mwovu?

Au kuwaambia wakuu, Ninyi ni wabaya?

19Sembuse huyo asiyependelea nyuso za wakuu,[#Kum 10:17]

Wala hawajali matajiri kuliko maskini?

Kwani wote ni kazi ya mikono yake,

20Hufa ghafula, hata usiku wa manane;

Watu hutikisika na kwenda zao,

Nao mashujaa huondolewa pasipo mkono wa mtu.

21Kwani macho yake ya juu ya njia za mtu,

Naye huiona miendo yake yote.

22Hapana weusi, wala hilo giza tupu,

Wawezapo kujificha watendao udhalimu.

23Kwani yeye hana haja ya kumfikiria mtu zaidi,[#Ezr 9:13]

ili aende mbele za Mungu ahukumiwe.

24Yeye huwavunja-vunja mashujaa pasina kuwachunguza,

Na kuwaweka wengine mahali pao.

25Kwa sababu hiyo yeye huyatafiti matendo yao;

Naye huwapindia usiku, wakaangamia.

26Yeye huwapiga kama watu wabaya

Waziwazi mbele ya macho ya wengine;

27Kwa sababu walikengeuka, wasimwandame yeye,

Wasikubali kuzishika njia zake hata moja;

28Hata wakafanya kilio cha maskini kumfikilia,[#Mhu 5:8; Yak 5:4; Kut 22:23; Zab 34:17; Mhu 3:16,17]

Naye akasikia kilio cha hao wateswao.

29Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa?

Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama?

Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa;

30Kwamba huyo mpotovu asitawale,[#Mit 29:2-12; 1 Fal 12:28-30]

Pasiwe na wa kuwatega watu.

31Kwani kuna mtu aliyemwambia Mungu,

Mimi nimevumilia kurudiwa, ingawa sikukosa;

32Nisiyoyaona nifundishe wewe;

Kama nimefanya uovu sitafanya tena?

33Je! Malipo yake yatakuwa kama upendavyo wewe, hata ukayakataa?

Kwani yakupasa wewe kuchagua, si mimi;

Kwa sababu hiyo sema uyajuayo.

34Watu walio na akili wataniambia,

Naam, kila mtu mwenye hekima anisikiaye;

35Huyo Ayubu amesema pasipo maarifa,[#Ayu 38:2]

Na maneno yake hayana hekima.

36Laiti Ayubu angejaribiwa hata mwisho,

Kwa kuwa amejibu kama watu waovu.

37Kwani huongeza uasi juu ya dhambi zake,

Apiga makofi kati yetu,

Na kuongeza maneno yake kinyume cha Mungu.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania