Ayu 40

Ayu 40

1BWANA akafuliza kumjibu Ayubu, na kusema,

2Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi?[#Ayu 9:3; Isa 45:9]

Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.

Jibu la Ayubu kwa Mungu

3Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema,

4Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini?[#Ezr 9:6; Zab 51:4; Ayu 29:9; Zab 39:9; Zek 2:13]

Naweka mkono wangu kinywani pangu.

5Nimenena mara moja, nami sitajibu;

Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.

Mungu Amchochea Ayubu

6Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,[#Ayu 38:1; Zab 50:3]

7Jifunge viuno kama mwanamume,[#Ayu 38:3; 42:4]

Mimi nitakuuliza neno, nawe niambie.

8Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha?[#Zab 51:4]

Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki?

9Au je! Wewe una mkono kama Mungu?[#Ayu 37:4; Zab 29:3]

Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye?

10Haya! Jivike sasa fahari na ukuu;[#Zab 93:1]

Jipambe heshima na enzi.

11Mwaga mafuriko ya hasira zako,

Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhili.

12Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe,[#Isa 2:12; Dan 4:37; Lk 18:14]

Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo.

13Wafiche mavumbini pamoja,

Wafunge nyuso zao mahali palipositirika.

14Ndipo mimi nami nitazikiri habari zako,

Ya kuwa mkono wako wa kuume waweza kukuokoa.

15Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe;

Yeye hula nyasi kama vile ng’ombe,

16Tazama basi, nguvu zake ni katika viuno vyake,

Na uwezo wake u katika mishipa ya tumbo lake.

17Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi;

Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.

18Mifupa yake ni kama mirija ya shaba;

Mbavu zake ni kama vipande vya chuma.

19Yeye ni mkuu wa njia za Mungu;

Yeye aliyemfanya alimpa upanga wake.

20Hakika milima humtolea chakula;[#Zab 104:14]

Hapo wachezapo wanyama wote wa barani.

21Hulala chini ya miti yenye vivuli,

Mafichoni penye mianzi, na matopeni.

22Hiyo miti yenye vivuli humfunika kwa vivuli vyao;

Mierebi ya vijito humzunguka.

23Tazama, mto ukifurika, yeye hatetemeki;[#Mwa 13:10; Yer 12:5]

Hujiona yu salama, ijapokuwa Yordani hufurika hata kinywani pake.

24Je! Mtu ye yote atamnasa akiwa yu macho,

Au, kumtoboa pua yake kwa mtego?

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania