The chat will start when you send the first message.
1Basi ilikuwa siku ya nane, Musa akawaita Haruni na wanawe, pamoja na wazee wa Israeli;[#Law 14:10,23; Eze 43:27]
2akamwambia Haruni, Twaa wewe mwana-ng’ombe mume awe sadaka ya dhambi, na kondoo mume wa sadaka ya kuteketezwa, wakamilifu, ukawasongeze mbele ya BWANA.[#Kut 29:1; Law 4:3; 8:14,18]
3Nawe utawaambia wana wa Israeli, ukisema, Twaeni mbuzi mume awe sadaka ya dhambi; na mwana-ng’ombe, na mwana-kondoo, wote wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, kwa sadaka ya kuteketezwa;[#Law 4:23; 10:19; Ezr 6:17; Isa 53:10; Rum 8:3; 1 Pet 2:24]
4na ng’ombe mume, na kondoo mume, kwa sadaka za amani, ili kuwachinja mbele za BWANA; na sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta; kwa maana, BWANA hivi leo atawatokea.[#Law 2:4; Kut 29:43]
5Nao wakayaleta hayo yaliyoagizwa na Musa wakayaweka mbele ya hema ya kukutania; kisha mkutano wote ukakaribia wakasimama mbele za BWANA.
6Kisha Musa akasema, Neno aliloliagiza BWANA kwamba mlifanye ni hili; na huo utukufu wa BWANA utawatokea.[#Kut 24:16; 40:34,35; 1 Fal 8:10-12]
7Musa akamwambia Haruni, Ikaribie madhabahu, uitoe sadaka yako ya dhambi, na sadaka yako ya kuteketezwa, ukafanye upatanisho kwa ajili ya nafsi yako, na kwa ajili ya watu; nawe uitoe hiyo dhabihu ya watu, ukafanye upatanisho kwa ajili yao; kama BWANA alivyoagiza.[#Ebr 5:1,3; 7:27; 9:7; 1 Sam 3:14; Law 4:16,20]
8Basi Haruni akakaribia madhabahuni, akamchinja huyo mwana-ng’ombe wa sadaka ya dhambi, aliyekuwa kwa ajili ya nafsi yake.
9Kisha wana wa Haruni wakamsongezea Haruni ile damu; naye akatia kidole chake katika damu, na kuitia katika pembe za madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu;[#Law 8:15; 4:7]
10lakini mafuta, na figo, na kitambi kilichotoka katika ini ya hiyo sadaka ya dhambi, akaviteketeza juu ya madhabahu, kama BWANA alivyomwagiza Musa.[#Law 8:16; 4:8]
11Na nyama, na ngozi akazichoma moto nje ya marago.[#Law 4:10,11; 8:17]
12Naye akaichinja sadaka ya kuteketezwa; na wanawe Haruni wakamsongezea ile damu, naye akainyunyiza katika madhabahu pande zote.
13Nao wakamletea sadaka ya kuteketezwa kipande kwa kipande, na kichwa; naye akaviteketeza juu ya madhabahu.
14Kisha akaosha matumbo, na miguu na kuiteketeza juu ya hiyo sadaka ya kuteketezwa madhabahuni.
15Kisha akaisongeza dhabihu ya watu, akamtwaa mbuzi wa sadaka ya dhambi aliyekuwa kwa hao watu, na kumchinja, na kumtoa kwa ajili ya dhambi kama yule wa kwanza.[#Isa 53:10; Yn 1:29; 1 Kor 15:3; 2 Kor 5:21; Efe 5:2; Gal 1:4; Ebr 1:3; 2:17; 1 Pet 2:24; 3:18; 1 Yoh 2:2; 4:10; Ufu 1:5]
16Kisha akaisongeza sadaka ya kuteketezwa, na kuitoa sawasawa na sheria.
17Kisha akaisongeza sadaka ya unga, na kutwaa konzi humo, na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi.[#Kut 29:38]
18Huyo ng’ombe mume naye akamchinja, na huyo kondoo mume pia, dhabihu ya sadaka za amani, zilizokuwa kwa ajili ya watu; na wanawe Haruni wakamsongezea ile damu, naye akainyunyiza katika madhabahu pande zote,[#Law 3:1-11]
19na mafuta ya ng’ombe; na ya kondoo, mkia wake wa mafuta, na hayo yafunikayo matumbo, na figo zake, na kitambi cha ini;
20nao wakayaweka hayo mafuta juu ya vidari, naye akayateketeza mafuta juu ya madhabahu;
21na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kuume, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA; kama Musa alivyoagiza.[#Kut 29:24]
22Kisha Haruni akainua mikono yake na kuielekeza kwa hao watu, akawabariki; kisha akashuka akisha isongeza sadaka ya dhambi, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani.[#Hes 6:22-26; Kum 21:5; Lk 24:50]
23Kisha Musa na Haruni wakaingia ndani ya hema ya kukutania, kisha wakatoka nje, na kuwabarikia watu; na huo utukufu wa BWANA ukawatokea watu wote.[#2 Sam 6:18; 2 Nya 6:3; 1 Nya 16:2; Hes 16:19]
24Kisha moto ukatoka hapo mbele za BWANA, na kuiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na yale mafuta juu ya madhabahu; watu wote walipouona huo moto wakapiga kelele wakainama kifudifudi.[#Mwa 4:4; 15:17; 2 Nya 7:1; Kut 29:18; 1 Fal 18:39; Ezr 3:11]