Hes 12

Hes 12

Haruni na Miriamu Wamwonea Wivu Musa

1Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.[#Kut 2:21]

2Wakasema, Je! Ni kweli BWANA amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? BWANA akasikia maneno yao.[#Kut 15:20; Mik 6:4; Mwa 29:33; 2 Fal 19:4; Zab 94:9; Isa 37:4; Eze 35:12]

3Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.[#Zab 147:6; 149:4; Mt 5:5; 21:5; 1 Tim 6:11; 2 Tim 2:25; 1 Pet 3:4]

4BWANA akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje.[#Zab 76:9]

5BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.[#Kut 34:5; 40:38; Hes 16:19]

6Kisha akawaambia,[#Mwa 46:2; Ayu 33:15; Lk 1:11,22; Mt 1:20]

Sikizeni basi maneno yangu;

Akiwapo nabii kati yenu,

Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono,

Nitasema naye katika ndoto.

7Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa;[#Ebr 3:2,5; Zab 105:26]

Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;

8Kwake nitanena mdomo kwa mdomo,[#Kut 33:11; Kum 34:10; 1 Kor 13:12; Kut 33:19; 2 Pet 2:10]

Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo;

Na umbo la BWANA yeye ataliona.

Mbona basi ninyi hamkuogopa

Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?

9Hasira za BWANA zikawaka juu yao; naye akaenda zake.

10Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.[#Kum 24:9; 2 Fal 5:27; 2 Nya 26:19]

11Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.[#2 Sam 19:19]

12Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake.[#Zab 88:4; Efe 2:1-5; Kol 2:13; 1 Tim 5:6]

13Musa akamlilia BWANA, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana.[#Yak 5:16]

14BWANA akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena.[#Hes 5:2-3; Ebr 12:9; Law 13:46; 14:8; 2 Nya 26:20,21]

15Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena.[#Kum 24:9; 2 Nya 26:20]

16Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga kambi katika nyika ya Parani.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania