The chat will start when you send the first message.
1Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule.
2Kisha wana wa Israeli wote wakamnung’unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.[#Zab 106:25; Kum 28:68]
3Mbona BWANA anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri?
4Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe akida, tukarudi Misri.[#Neh 9:17; Mdo 7:39; Ebr 11:15]
5Ndipo Musa na Haruni wakaanguka kifudifudi mbele ya mkutano wa kusanyiko la wana wa Israeli.
6Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao;
7wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu.
8Ikiwa BWANA anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali.[#Kum 10:15; 2 Sam 15:25; 1 Fal 10:9; Zab 22:8; Isa 62:4; Hes 13:27]
9Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye BWANA yu pamoja nasi; msiwaogope.[#Ebr 3:16; Kum 9:7,23,24; Kum 20:3; Hes 24:8; Mwa 48:21; Kut 33:16; Kum 20:1; 2 Nya 15:2; Isa 41:10]
10Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa BWANA ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote.[#Kut 17:4; 16:10; Law 9:23]
11BWANA akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao.[#Ebr 3:8; Zab 78:22; Yn 12:37]
12Nitawapiga kwa tauni, na kuwaondolea urithi wao, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, kisha yenye nguvu kuliko wao.[#Kut 32:10]
13Basi Musa akamwambia BWANA, Ndipo Wamisri watasikia habari hiyo; kwa kuwa wewe uliwaleta watu hawa kwa uweza wako, kutoka kati yao;[#Kut 32:11-14; Eze 20:9]
14kisha watawaambia wenyeji wa nchi hii; wamesikia wao ya kuwa wewe BWANA u kati ya watu hawa; maana, wewe BWANA waonekana uso kwa uso, na wingu lako lasimama juu yao, kisha wewe watangulia mbele yao, katika nguzo ya wingu mchana, na katika nguzo ya moto usiku.[#Kut 15:14; Neh 9:12]
15Basi kama wewe ukiwaua watu hawa mfano wa mtu mmoja, ndipo mataifa yaliyosikia habari za sifa zako watakaponena na kusema,
16Ni kwa sababu yeye BWANA hakuweza kuwaleta watu hao kuwatia katika nchi aliyowaapia, kwa ajili ya hayo amewaua nyikani.[#Yos 7:9]
17Basi sasa nakusihi sana, uweza wa Bwana wangu na uwe mkuu, kama ulivyonena, uliposema,
18BWANA ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yo yote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne.[#Kut 20:5-6; 34:6-7; Kum 5:9-10; 7:9-10; Zab 103:8; 145:8; Yon 4:2; Kut 34:7]
19Nakusihi, usamehe uovu wa watu hawa, kama ukuu wa rehema yako ulivyo, kama ulivyowasamehe watu hawa, tangu huko Misri hata hivi sasa.
20BWANA akasema, Mimi nimewasamehe kama neno lako lilivyokuwa;[#Yak 5:16; 1 Yoh 5:14]
21lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa BWANA;[#Ebr 3:18; Zab 72:19; Isa 5:16; 11:9; 61:11; Eze 18:3; Hab 2:14; Ufu 11:15]
22kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu;[#Kum 1:31,34; Zab 95:11; Ebr 4:6,7; Mwa 31:7]
23hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona;[#Kum 1:35; Zab 106:26; Eze 20:15; Ebr 3:18; 4:3]
24lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na uzao wake wataimiliki.[#Yos 14:9-12; Zab 25:13; Isa 33:15; Mt 5:5]
25Basi Mwamaleki na Mkanaani wakaa katika bonde; kesho geukeni, mkaende jangwani kwa njia iendayo Bahari ya Shamu.
26Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
27Je! Nichukuane na mkutano mwovu huu uninung’unikiao hata lini? Nimesikia manung’uniko ya wana wa Israeli, waninung’unikiayo.[#Kut 16:28; Mt 17:17; Mk 9:19; Kut 16:12; 1 Kor 10:10]
28Waambieni, Kama niishivyo, asema BWANA, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi;[#Ebr 3:17]
29mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung’unikia,[#Hes 26:64]
30hakika yangu hamtaingia ninyi katika nchi, ambayo niliinua mkono wangu ya kwamba nitawaketisha humo, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.[#Kum 1:36,38]
31Lakini Watoto wenu, ambao mlisema watakuwa mateka, ndio nitakaowaleta na kuwatia ndani, nao wataijua nchi ninyi mliyoikataa.[#Zab 106:24; Mit 1:25,26; Ebr 12:16,17]
32Lakini katika habari zenu, mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili.[#1 Kor 10:5]
33Kisha watoto wenu watakuwa wachungaji jangwani muda wa miaka arobaini nao watauchukua mzigo wa uasherati wenu, hata mizoga yenu itakapoangamia jangwani.[#Mdo 7:36; Zab 107:40; Kum 2:14]
34Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu.[#Hes 13:25; Zab 95:10; Eze 4:6; 1 Fal 8:56; Zab 77:8; Ebr 4:1]
35Mimi BWANA nimekwisha nena, hakika yangu ndilo nitakaloutenda mkutano mwovu huu wote, waliokusanyika juu yangu; wataangamia katika nyika hii, nako ndiko Watakakokufa.[#Hes 23:19]
36Kisha hao watu, ambao Musa aliwatuma waipeleleze nchi, waliorudi, na kufanya mkutano wote kumnung’unikia, kwa walivyoleta habari mbaya juu ya nchi,[#Hes 13:31]
37watu hao walioileta habari mbaya ya nchi wakafa kwa tauni mbele ya BWANA.[#Yer 28:16,17; 1 Kor 10:10; Ebr 3:17; Yud 1:5]
38Lakini Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, wakabaki hai miongoni mwa wale watu waliokwenda kuipeleleza nchi.[#Yos 14:6]
39Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli wote maneno haya, na hao watu wakaombolea sana.[#Mit 19:3; Mt 8:12; Ebr 12:17]
40Wakainuka na mapema asubuhi, wakakwea juu ya mlima hata kileleni, wakisema, Tazameni, sisi tupo hapa, nasi tutakwea kwenda mahali BWANA alipotuahidi; kwani tumefanya dhambi.[#Kum 1:41; Mhu 9:3; Mt 7:21; Lk 13:25]
41Musa akawaambia, Kwa nini ninyi sasa kuyahalifu maagizo ya BWANA? Maana halitafanikiwa jambo hilo.[#2 Nya 24:20; Ayu 9:4; Isa 59:1,2; Yer 2:37; 1 Kor 10:22]
42Msikwee, kwa kuwa BWANA hamo kati yenu; msipigwe na kuangushwa mbele ya adui zenu.[#Kum 1:42; Zab 44:1-3]
43Kwa kuwa Mwamaleki na Mkanaani wako mbele yenu, nanyi mtaanguka kwa upanga, kwa sababu mmerudi nyuma msimwandame BWANA, kwa hiyo BWANA hatakuwa pamoja nanyi.[#Kum 1:43,44; Amu 16:20]
44Lakini walithubutu kukwea mlimani hata kileleni; ila sanduku la agano la BWANA halikutoka humo maragoni, wala Musa hakutoka.
45Ndipo Mwamaleki, na Mkanaani waliokaa huko mlimani, wakatelemka, wakawapiga na kuwaangusha, hata kufikilia Horma.