Mit 26

Mit 26

1Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno;[#Zab 12:8]

Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu.

2Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,[#Hes 23:8]

Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake;

Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.

3Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda,

Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu.

4Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;[#Isa 36:21]

Usije ukafanana naye.

5Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;

Asije akawa mwenye hekima machoni pake.

6Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu

Hujikata miguu, na kunywa hasara.

7Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu;

Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.

8Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe;

Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu.

9Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi;

Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.

10Fundi stadi hufanyiza vitu vyote;

Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao.

11Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake;[#2 Pet 2:22]

Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.

12Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe?

Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.

13Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani,

Simba yuko katika njia kuu.

14Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake;

Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake.

15Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini;

Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake.

16Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake,

Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu.

17Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake;

Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake.

18Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge,

Na mishale, na mauti;

19Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake,[#Efe 5:4]

Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu?

20Moto hufa kwa kukosa kuni;

Na bila mchongezi fitina hukoma.

21Kama makaa juu ya makaa yanayowaka,[#2 Sam 20:1]

Na kama kuni juu ya moto;

Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui.

22Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo.[#Eze 22:9]

Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.

23Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbaya[#Lk 22:48]

Ni kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha.

24Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake;

Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake.

25Anenapo maneno mazuri usimsadiki;

Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake.

26Ingawa chuki hufunikizwa kwa hila;

Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko.

27Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe;[#Est 7:10]

Naye abingirishaye jiwe litamrudia.

28Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi;[#Mit 13:6]

Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania