The chat will start when you send the first message.
1Mwanangu, sikiliza hekima yangu;
Tega sikio lako, mzisikie akili zangu;
2Upate kuilinda busara,[#Mal 2:7]
Na midomo yako iyahifadhi maarifa.
3Maana midomo ya malaya hudondoza asali,
Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
4Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga;[#Mhu 7:26; Ebr 4:12]
Ni mkali kama upanga wa makali kuwili.
5Miguu yake inatelemkia mauti;[#Ebr 13:4]
Hatua zake zinashikamana na kuzimu;
6Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima;
Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari.
7Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,
Wala msiache maneno ya kinywa changu.
8Itenge njia yako mbali naye,
Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.
9Usije ukawapa wengine heshima yako,
Na wakorofi miaka yako;
10Wageni wasije wakashiba nguvu zako;
Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;
11Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho,
Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;
12Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo,
Na moyo wangu ukadharau kukemewa;
13Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu,
Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha!
14Nalikuwa karibu na kuingia katika maovu yote,
Katikati ya mkutano na kusanyiko.
15Unywe maji ya birika lako mwenyewe,
Na maji yenye kububujika katika kisima chako.
16Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali,
Na mito ya maji katika njia kuu?
17Yawe yako mwenyewe peke yako,
Wala si ya wageni pamoja nawe.
18Chemchemi yako ibarikiwe;[#Mhu 9:9; Mal 2:14]
Nawe umfurahie mke wa ujana wako.
19Ni ayala apendaye na paa apendezaye;[#Wim 2:9]
Maziwa yake yakutoshe sikuzote;
Na kwa upendo wake ushangilie daima.
20Mwanangu! Mbona unashangilia malaya,
Na kukikumbatia kifua cha mgeni?
21Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya BWANA,[#2 Nya 16:9; Ayu 31:4; Yer 16:17; Hos 7:2; Ebr 4:13]
Na mienendo yake yote huitafakari.
22Maovu yake yeye yatampata mdhalimu,[#Zab 9:15]
Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.
23Atakufa huyo kwa kukosa maonyo,[#Ayu 4:21; Mit 10:21]
Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.