The chat will start when you send the first message.
1Heri mtu yule asiyekwenda[#Mwa 5:24; Ayu 31:5; Zab 81:12; Mit 4:14]
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3Naye atakuwa kama mti uliopandwa[#Yer 17:8; Mwa 39:3; Zab 128:2]
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.
4Sivyo walivyo wasio haki;
Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,
Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.
6Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki,[#Nah 1:7; Yn 10:14]
Bali njia ya wasio haki itapotea.