The chat will start when you send the first message.
1Rehema na hukumu nitaziimba,
Ee BWANA, nitakuimbia zaburi.
2Nitaiangalia njia ya unyofu;[#1 Sam 18:14; Mwa 18:19; Kum 6:7; 1 Fal 9:4]
Utakuja kwangu lini?
Nitakwenda kwa unyofu wa moyo
Ndani ya nyumba yangu.
3Sitaweka mbele ya macho yangu[#Yos 23:6; 1 Sam 12:20]
Neno la uovu.
Kazi yao waliopotoka naichukia,
Haitaambatana nami.
4Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu,[#Mt 7:23; 1 Kor 5:11; 2 Tim 2:19]
Lililo ovu sitalijua.
5Amsingiziaye jirani yake kwa siri,[#Mit 6:17; Lk 18:14]
Huyo nitamharibu.
Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno,
Huyo sitavumilia naye.
6Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,[#Rum 13:4]
Hao wakae nami.
Yeye aendaye katika njia kamilifu,
Ndiye atakayenitumikia.
7Hatakaa ndani ya nyumba yangu
Mtu atendaye hila.
Asemaye uongo hatathibitika
Mbele ya macho yangu.
8Asubuhi hata asubuhi nitawaharibu[#Yer 21:12; Hos 9:3]
Wabaya wote wa nchi.
Niwatenge wote watendao uovu
Na mji wa BWANA.