The chat will start when you send the first message.
1Haleluya.
Heri mtu yule amchaye BWANA,
Apendezwaye sana na maagizo yake.
2Wazao wake watakuwa hodari duniani;
Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.
3Nyumbani mwake mna utajiri na mali,[#Mit 3:16; 15:6; Isa 33:6; Mt 6:33; 2 Kor 6:10]
Na haki yake yakaa milele.
4Nuru huwazukia wenye adili gizani;
Ana fadhili na huruma na haki.
5Heri atendaye fadhili na kukopesha;[#Lk 6:35]
Atengenezaye mambo yake kwa haki.
6Kwa maana hataondoshwa kamwe;
Mwenye haki atakumbukwa milele.
7Hataogopa habari mbaya;
Moyo wake u imara ukimtumaini BWANA.
8Moyo wake umethibitika hataogopa,
Hata awaone watesi wake wameshindwa.
9Amekirimu, na kuwapa maskini,[#Lk 11:41; Rum 12:13; Mdo 4:35; 20:35; 2 Kor 8:9; 9:9; 1 Tim 6:18]
Haki yake yakaa milele,
Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
10Asiye haki ataona na kusikitika,[#Lk 13:28]
Atasaga meno yake na kuyeyuka,
Tamaa ya wasio haki itapotea.