Zab 113

Zab 113

Mungu Msaidizi wa Mhitaji

1Haleluya.

Enyi watumishi wa BWANA, sifuni,

Lisifuni jina la BWANA.

2Jina la BWANA lihimidiwe[#Dan 2:20]

Tangu leo na hata milele.

3Toka maawio ya jua hata machweo yake[#Isa 59:19; Hab 2:14; Mal 1:11; Ufu 11:15]

Jina la BWANA husifiwa.

4BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,

Na utukufu wake ni juu ya mbingu.

5Ni nani aliye mfano wa BWANA,

Mungu wetu aketiye juu;

6Anyenyekeaye kutazama,[#Isa 57:15]

Mbinguni na duniani?

7Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,[#1 Sam 2:8; Isa 26:19; Dan 12:2]

Na kumpandisha maskini kutoka jaani.

8Amketishe pamoja na wakuu,[#Ayu 36:7]

Pamoja na wakuu wa watu wake.

9Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa,[#1 Sam 2:5; Gal 4:27]

Awe mama ya watoto mwenye furaha.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania