The chat will start when you send the first message.
1Haleluya.[#Kut 12:51]
Israeli alipotoka Misri,
Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
2Yuda ilikuwa patakatifu pake,
Israeli milki yake.
3Bahari iliona ikakimbia,[#Kut 14:21; Yos 3:16]
Yordani ilirudishwa nyuma.
4Milima iliruka kama kondoo waume,[#Zab 29:6; 68:16; Hab 3:6]
Vilima kama wana-kondoo.
5Ee bahari, una nini, ukimbie?
Yordani, urudi nyuma?
6Enyi milima, mruke kama kondoo waume?
Enyi vilima, kama wana-kondoo?
7Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana,
Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.
8Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji,[#Kut 17:1-7; Hes 20:2-13; Zab 107:35]
Jiwe gumu kuwa chemchemi.