The chat will start when you send the first message.
1Haleluya.
Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza
Sauti yangu na dua zangu.
2Kwa maana amenitegea sikio lake,
Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.
3Kamba za mauti zilinizunguka,
Shida za kuzimu zilinipata.
Naliona taabu na huzuni;
4Nikaliitia jina la BWANA.
Ee BWANA, nakuomba sana,
Uniokoe nafsi yangu.
5BWANA ni mwenye neema na haki,[#Ezr 9:15; Neh 9:8; Zab 11:7; Yer 12:1; Omb 1:18; Ufu 16:5]
Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.
6BWANA huwalinda wasio na hila;
Nalidhilika, akaniokoa.
7Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako,[#Yer 6:16; Mt 11:29]
Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu.
8Maana umeniponya nafsi yangu na mauti,
Macho yangu na machozi,
Na miguu yangu na kuanguka.
9Nitaenenda mbele za BWANA
Katika nchi za walio hai.
10Naliamini, kwa maana nitasema,[#2 Kor 4:13]
Mimi naliteswa sana.
11Mimi nalisema kwa haraka yangu,[#2 Fal 4:16; Yer 9:5; Rum 3:4]
Wanadamu wote ni waongo.
12Nimrudishie BWANA nini
Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
13Nitakipokea kikombe cha wokovu;
Na kulitangaza jina la BWANA;
14Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,[#Zab 22:25; Yon 2:6]
Naam, mbele ya watu wake wote.
15Ina thamani machoni pa BWANA[#Ayu 5:26; Zab 72:14; Lk 16:22; Ufu 14:13]
Mauti ya wacha Mungu wake.
16Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako,
Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako,
Umevifungua vifungo vyangu.
17Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;
Na kulitangaza jina la BWANA;
18Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,
Naam, mbele ya watu wake wote.
19Katika nyua za nyumba ya BWANA,
Ndani yako, Ee Yerusalemu.