Zab 12

Zab 12

Ombi la Msaada Wakati wa Dhiki

1BWANA, uokoe, maana mcha Mungu amekoma,[#Isa 57:1]

Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.

2Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe,

Wenye midomo ya kujipendekeza;

Husemezana kwa mioyo ya unafiki;

3BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza,

Nao ulimi unenao maneno ya kiburi;

4Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda;

Midomo yetu ni yetu wenyewe,

Ni nani aliye bwana juu yetu?

5Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge,[#Kut 3:7,8]

Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji,

Sasa nitasimama, asema BWANA,

Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.

6Maneno ya BWANA ni maneno safi,[#2 Sam 22:31; Zab 18:30; Mit 30:5]

Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi;

Iliyosafishwa mara saba.

7Wewe, BWANA, ndiwe utakayetuhifadhi,

Utatulinda na kizazi hiki milele.

8Wasio haki hutembea pande zote,

Ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania