The chat will start when you send the first message.
1Katika shida yangu nalimlilia BWANA
Naye akaniitikia.
2Ee BWANA, uiponye nafsi yangu
Na midomo ya uongo na ulimi wa hila.
3Akupe nini, akuzidishie nini,
Ewe ulimi wenye hila?
4Mishale ya mtu hodari iliyochongoka,
Pamoja na makaa ya mretemu.
5Ole wangu mimi![#Mwa 10:2; 1 Sam 25:1; Yer 49:28]
Kwa kuwa nimekaa katika Mesheki;
Na kufanya maskani yangu
Katikati ya hema za Kedari.
6Nafsi yangu imekaa siku nyingi,
Pamoja naye aichukiaye amani.
7Mimi ni wa amani;
Bali ninenapo, wao huelekea vita.