The chat will start when you send the first message.
1Nitayainua macho yangu niitazame milima,
Msaada wangu utatoka wapi?
2Msaada wangu u katika BWANA,
Aliyezifanya mbingu na nchi.
3Asiuache mguu wako usogezwe;[#1 Sam 2:9; Isa 27:3]
Asisinzie akulindaye;
4Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi,
Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5BWANA ndiye mlinzi wako;
BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.
6Jua halitakupiga mchana,[#Isa 49:10]
Wala mwezi wakati wa usiku.
7BWANA atakulinda na mabaya yote,[#Ayu 5:19; Zab 91:9,10; Mit 12:21]
Atakulinda nafsi yako.
8BWANA atakulinda utokapo na uingiapo,[#Kum 28:6; Mit 2:8]
Tangu sasa na hata milele.