The chat will start when you send the first message.
1Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,[#Mwa 15:1; Hes 14:9; Yos 1:5; Ebr 13:5; Rum 8:31]
Israeli na aseme sasa,
2Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,
Wanadamu walipotushambulia.
3Papo hapo wangalitumeza hai,[#Zab 35:25; Mit 1:12; Yer 51:34]
Hasira yao ilipowaka juu yetu
4Papo hapo maji yangalitugharikisha,
Mto ungalipita juu ya roho zetu;
5Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu
Maji yafurikayo.
6Na ahimidiwe BWANA;
Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.
7Nafsi yetu imeokoka kama ndege
Katika mtego wa wawindaji,
Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.
8Msaada wetu u katika jina la BWANA,[#Kut 18:4; Zab 12:2; Mit 18:10; Isa 50:10; Ebr 13:6]
Aliyezifanya mbingu na nchi.