The chat will start when you send the first message.
1BWANA asipoijenga nyumba
Waijengao wafanya kazi bure.
BWANA asipoulinda mji
Yeye aulindaye akesha bure.
2Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema,[#Mwa 3:17]
Na kukawia kwenda kulala,
Na kula chakula cha taabu;
Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
3Tazama, wana ndio urithi wa BWANA,[#Mwa 33:5; Kum 28:4]
Uzao wa tumbo ni thawabu.
4Kama mishale mkononi mwa shujaa,
Ndivyo walivyo wana wa ujanani.
5Heri mtu yule
Aliyelijaza podo lake hivyo.
Naam, hawataona aibu
Wanaposema na adui langoni.