The chat will start when you send the first message.
1Heri kila mtu amchaye BWANA,
Aendaye katika njia yake.
2Taabu ya mikono yako hakika utaila;[#Isa 3:10]
Utakuwa heri, na kwako kwema.
3Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,
Vyumbani mwa nyumba yako.
Wanao kama miche ya mizeituni
Wakiizunguka meza yako.
4Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA.
5BWANA akubariki toka Sayuni;[#Zab 134:3]
Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
6Naam, ukawaone wana wa wanao.[#Mwa 50:23]
Amani ikae na Israeli.