The chat will start when you send the first message.
1BWANA, umkumbukie Daudi
Taabu zake zote alizotaabika.
2Ndiye aliyemwapia BWANA,
Akaweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo.
3Sitaingia hemani mwa nyumba yangu,
Wala sitapanda matandiko ya kitanda changu;
4Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi,[#Rut 3:18]
Wala kope zangu kusinzia;
5Hata nitakapompatia BWANA mahali,
Na Shujaa wa Yakobo maskani.
6Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata,[#Yos 18:1; 1 Nya 13:5; 2 Nya 6:41-42; 1 Sam 17:12; 7:1]
Katika konde la Yearimu tuliiona.
7Na tuingie katika maskani yake,
Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake.
8Ee BWANA, uinuke, uende kwenye raha yako,[#Hes 10:35]
Wewe na sanduku la nguvu zako.
9Makuhani wako na wavikwe haki,[#Ayu 29:14; Isa 61:10]
Watauwa wako na washangilie.
10Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako,
Usiurudishe nyuma uso wa masihi wako.
11BWANA amemwapia Daudi neno la kweli,[#1 Fal 8:25; 2 Sam 7:12-16; 1 Nya 6:16; 1 Nya 17:11-14; Zab 89:4-5; Lk 1:69; Mdo 2:30]
Hatarudi nyuma akalihalifu,
Baadhi ya wazao wa mwili wako
Nitawaweka katika kiti chako cha enzi.
12Wanao wakiyashika maagano yangu,
Na shuhuda nitakazowafundisha;
Watoto wao nao wataketi
Katika kiti chako cha enzi milele.
13Kwa kuwa BWANA ameichagua Sayuni,
Ameitamani akae ndani yake.
14Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele,
Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani.
15Hakika nitavibariki vyakula vyake
Wahitaji wake nitawashibisha chakula.
16Na makuhani wake nitawavika wokovu,[#2 Nya 6:41; Hos 11:12]
Na watauwa wake watashangilia.
17Hapo nitamchipushia Daudi pembe,[#1 Fal 11:36; Zab 92:10; Eze 29:21; Lk 1:69]
Na taa nimemtengenezea masihi wangu.
18Adui zake nitawavika aibu,
Bali juu yake taji yake itasitawi.