The chat will start when you send the first message.
1Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza,[#Mwa 13:8; 1 Kor 1:10]
Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.
2Ni kama mafuta mazuri kichwani,[#Kut 30:25]
Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni,
Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.
3Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni.[#Kum 4:48; 28:8; Law 25:11; Dan 12:2,3; Mt 25:34,46; Yn 4:14; 17:3; Ebr 7:25; 1 Yoh 5:20]
Maana ndiko BWANA alikoamuru baraka,
Naam, uzima hata milele.