The chat will start when you send the first message.
1Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;[#1 Nya 16:34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 100:5; 106:1; 107:1; 118:1; Yer 33:11]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2Mshukuruni Mungu wa miungu;[#Kut 18:11; Kum 10:17]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
3Mshukuruni Bwana wa mabwana;[#1 Tim 6:15; Ufu 17:14]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
4Yeye peke yake afanya maajabu makuu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
5Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake;[#Mwa 1:1; Mit 3:19]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
6Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji;[#Mwa 1:2; Yer 10:12]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
7Yeye aliyefanya mianga mikubwa;[#Mwa 1:16; Kum 4:19]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
8Jua litawale mchana;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
9Mwezi na nyota zitawale usiku;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
10Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao;[#Kut 12:29]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
11Akawatoa Waisraeli katikati yao;[#Kut 12:51]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
12Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
13Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu;[#Zab 78:13; Kut 14:21-29]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
14Akawavusha Israeli katikati yake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
15Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
16Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani;[#Kum 8:15]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
17Yeye aliyewapiga wafalme wakuu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
18Akawaua wafalme mashuhuri;[#Kum 29:7]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
19Sihoni, mfalme wa Waamori;[#Hes 21:21-30]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
20Na Ogu, mfalme wa Bashani;[#Hes 21:31-35]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
21Akaitoa nchi yao iwe urithi;[#Yos 12:1]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
22Urithi wa Israeli mtumishi wake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
23Aliyetukumbuka katika unyonge wetu;[#Mwa 8:1; Kum 32:36; Zab 102:17; Isa 63:9; Lk 1:48]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
24Akatuokoa na watesi wetu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
25Kila chenye mwili akipa chakula chake;[#Zab 104:27]
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
26Mshukuruni Mungu wa mbingu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.