The chat will start when you send the first message.
1Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,[#Zab 119:46]
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
2Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu,[#1 Fal 8:29; Zab 5:7; Dan 6:10; Yon 2:7; Isa 42:21]
Nitalishukuru jina lako,
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa maana umeikuza ahadi yako,
Kuliko jina lako lote.
3Siku ile niliyokuita uliniitikia,[#2 Kor 12:9; Zek 10:12]
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
4Ee BWANA, wafalme wote wa dunia watakushukuru,
Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.
5Naam, wataziimba njia za BWANA,
Kwa maana utukufu wa BWANA ni mkuu.
6Ingawa BWANA yuko juu, amwona mnyenyekevu,[#Mit 3:34; Yak 4:6]
Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.
7Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha,[#Zab 23:3]
Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu,
Na mkono wako wa kuume utaniokoa.
8BWANA atanitimilizia mambo yangu;[#Zab 57:2; Flp]
Ee BWANA, fadhili zako ni za milele;
Usiziache kazi za mikono yako.