The chat will start when you send the first message.
1Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu,[#2 Sam 22:35]
Anifundishaye mikono yangu vita,
Vidole vyangu kupigana.
2Mhisani wangu na boma langu,
Ngome yangu na mwokozi wangu,
Ngao yangu niliyemkimbilia,
Huwatiisha watu wangu chini yangu.
3Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjue?[#Ayu 7:17-18; Zab 8:4; Ebr 2:6]
Na binadamu hata umwangalie?
4Binadamu amefanana na ubatili,
Siku zake ni kama kivuli kipitacho.
5BWANA, uziinamishe mbingu zako, ushuke,[#Isa 64:1]
Uiguse milima nayo itatoka moshi.
6Utupe umeme, uwatawanye,
Uipige mishale yako, uwafadhaishe.
7Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye,[#Zab 69:1; Mal 2:11]
Unitoe katika maji mengi, katika mkono wa wageni.
8Vinywa vyao vyasema visivyofaa,
Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
9Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,[#Zab 33:2]
Kwa kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.
10Awapaye wafalme wokovu,
Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.
11Uniponye, unitoe,
Katika mkono wa wageni.
Vinywa vyao vyasema visivyofaa,
Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
12Wana wetu na wawe kama miche
Waliokua ujanani.
Binti zetu kama nguzo za pembeni
Zilizonakishwa kwa kupamba hekalu.
13Ghala zetu na zijae
Zenye akiba za jinsi zote.
Kondoo zetu na wazae
Elfu na makumi elfu mashambani mwetu.
14Ng’ombe zetu na wachukue mizigo,[#Law 26:17]
Kusiwe na kushambuliwa.
Wala kusiwe na kuhamishwa,
Wala malalamiko katika njia zetu.
15Heri watu wenye hali hiyo,[#Kum 33:29]
Heri watu wenye BWANA kuwa Mungu wao.