Zab 149

Zab 149

Sifa kwa Wema wa Mungu kwa Israeli

1Haleluya.[#Isa 42:10]

Mwimbieni BWANA wimbo mpya,

Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.

2Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya,[#Ayu 35:10; Zek 9:9]

Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.

3Na walisifu jina lake kwa kucheza,

Kwa matari na kinubi wamwimbie.

4Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake,[#Mit 11:20]

Huwapamba wenye upole kwa wokovu.

5Watauwa na waushangilie utukufu,

Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.

6Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,[#Kum 7:1-2; Ebr 4:12; Ufu 1:16]

Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.

7Ili kufanya kisasi juu ya mataifa,

Na adhabu juu ya kabila za watu.

8Wawafunge wafalme wao kwa minyororo,

Na wakuu wao kwa pingu za chuma.

9Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa;[#Kum 7:1-2; Ufu 5:13; Rum 16:20; 1 Yoh 5:4]

Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote.

Haleluya.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania