The chat will start when you send the first message.
1Haleluya.
Msifuni Mungu katika patakatifu pake;
Msifuni katika anga la uweza wake.
2Msifuni kwa matendo yake makuu;
Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3Msifuni kwa mvumo wa baragumu;
Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4Msifuni kwa matari na kucheza;[#Kut 15:20; Isa 38:20]
Msifuni kwa zeze na filimbi;
5Msifuni kwa matoazi yaliayo;
Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.[#Ufu 5:13]
Haleluya.