Zab 26

Zab 26

Ombi la Haki na Ungamo la Wema

1Ee BWANA, unihukumu mimi,[#Zab 7:8; 28:7; Mit 29:25]

Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu,

Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.

2Ee BWANA, unijaribu na kunipima;

Unisafishe mtima wangu na moyo wangu.

3Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu,

Nami nimekwenda katika kweli yako.

4Sikuketi pamoja na watu wa ubatili,[#Zab 1:1; Yer 15:17]

Wala sitaingia mnamo wanafiki.

5Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya,[#Zab 5:5; 15:4; 31:6]

Wala sitaketi pamoja na watu waovu.

6Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia,[#Kut 30:19; Zab 73:13; 1 Tim 2:8]

Na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA

7Ili niitangaze sauti ya kushukuru,

Na kuzisimulia kazi zako za ajabu.

8BWANA, nimependa makao ya nyumba yako,

Na mahali pa maskani ya utukufu wako.

9Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji,

Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu.

10Mikononi mwao mna madhara,

Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa.

11Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu;

Unikomboe, unifanyie fadhili.

12Mguu wangu umesimama palipo sawa;

Katika makusanyiko nitamhimidi BWANA.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania