Zab 29

Zab 29

Sauti ya Mungu katika Dhoruba

1Mpeni BWANA, enyi wana wa Mungu,[#Zab 96:7-9; 1 Nya 16:28,29]

Mpeni BWANA utukufu na nguvu;

2Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;

Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.

3Sauti ya BWANA i juu ya maji;

Mungu wa utukufu alipiga radi;

BWANA yu juu ya maji mengi.

4Sauti ya BWANA ina nguvu;

Sauti ya BWANA ina adhama;

5Sauti ya BWANA yaivunja mierezi;

Naam, BWANA aivunja-vunja mierezi ya Lebanoni;

6Airusha-rusha kama ndama wa ng’ombe;[#Zab 114:4; Kum 3:9]

Lebanoni na Sirioni kama mwana-nyati.

7Sauti ya BWANA yaipasua miali ya moto;

8Sauti ya BWANA yalitetemesha jangwa;[#Hes 13:26]

BWANA alitetemesha jangwa la Kadeshi.

9Sauti ya BWANA yawazalisha ayala,

Na kuifichua misitu;

Na ndani ya hekalu lake

Wanasema wote, Utukufu.

10BWANA aliketi juu ya Gharika;[#Zab 93:4]

Naam, BWANA ameketi hali ya mfalme milele.

11BWANA atawapa watu wake nguvu;[#Isa 40:29]

BWANA atawabariki watu wake kwa amani.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania