Zab 3

Zab 3

Mwamini Mungu katika Dhiki

1BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,[#2 Sam 15:13—17:22]

Ni wengi wanaonishambulia,

2Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,[#2 Sam 16:8; Zab 22:7,8]

Hana wokovu huyu kwa Mungu.

3Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,[#2 Fal 25:27; Zab 27:6]

Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.

4Kwa sauti yangu namwita BWANA

Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.

5Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka,[#Zab 4:8; Mit 3:24; Mdo 12:6]

Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.

6Sitayaogopa makumi elfu ya watu,

Waliojipanga juu yangu pande zote.

7BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe,

Maana umewapiga taya adui zangu wote;

Umewavunja meno wasio haki.

8Wokovu una BWANA;[#Zab 37:39,40; Mit 21:31; Hes 13:4]

Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania