The chat will start when you send the first message.
1Nitamhimidi BWANA kila wakati,[#1 Sam 21:13-15]
Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
2Katika BWANA nafsi yangu itajisifu,[#Yer 9:24; 1 Kor 1:31]
Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
3Mtukuzeni BWANA pamoja nami,
Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
4Nalimtafuta BWANA akanijibu,[#Zab 18:6; Yon 2:2; Mt 7:7; Lk 11:9]
Akaniponya na hofu zangu zote.
5Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,
Wala nyuso zao hazitaona haya.
6Maskini huyu aliita, BWANA akasikia,[#Zab 3:4; 2 Sam 22:1]
Akamwokoa na taabu zake zote.
7Malaika wa BWANA hufanya kituo,[#Dan 6:22; Mwa 32:1; 2 Fal 6:17; Ebr 1:14]
Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
8Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema;[#1 Pet 2:3]
Heri mtu yule anayemtumaini.
9Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake,[#Flp 4:19]
Yaani, wamchao hawahitaji kitu.
10Wana-simba hutindikiwa, huona njaa;
Bali wamtafutao BWANA hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema.
11Njoni, enyi wana, mnisikilize,
Nami nitawafundisha kumcha BWANA.
12Ni nani mtu yule apendezwaye na uzima,[#1 Pet 3:10-12]
Apendaye siku nyingi apate kuona mema?
13Uuzuie ulimi wako na mabaya,[#1 Pet 2:22]
Na midomo yako na kusema hila.
14Uache mabaya ukatende mema,
Utafute amani ukaifuatie.
15Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki,[#Ayu 36:7]
Na masikio yake hukielekea kilio chao.
16Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya,[#Law 17:10; Yer 44:11; Mit 10:7]
Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
17Walilia, naye BWANA akasikia,
Akawaponya na taabu zao zote.
18BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na waliopondeka roho huwaokoa.
19Mateso ya mwenye haki ni mengi,
Lakini BWANA humponya nayo yote.
20Huihifadhi mifupa yake yote,[#Yn 19:36]
Haukuvunjika hata mmoja.
21Uovu utamwua asiye haki,[#Zab 94:23]
Nao wamchukiao mwenye haki watahukumiwa.
22BWANA huzikomboa nafsi za watumishi wake,[#2 Sam 4:9; Zab 103:4]
Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao.