The chat will start when you send the first message.
1Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake,[#Rum 3:18; Mwa 20:11; Mit 8:13; Mhu 12:3]
Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.
2Kwa maana hujipendekeza machoni pake
Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa.
3Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila,[#Yer 4:22]
Ameacha kuwa na akili na kutenda mema.
4Huwaza maovu kitandani pake,[#Mik 2:1; Isa 65:2]
Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii.
5Ee BWANA, fadhili zako zafika hata mbinguni,[#Zab 57:10]
Uaminifu wako hata mawinguni.
6Haki yako ni kama milima ya Mungu,[#Ayu 11:8; Rum 11:33; Ayu 7:20; Zab 145:9]
Hukumu zako ni vilindi vikuu,
Ee BWANA, unawaokoa wanadamu na wanyama.
7Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako![#Rut 2:12]
Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
8Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako,[#Ayu 20:17; Ufu 22:1]
Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.
9Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima,[#Isa 12:3; Yer 2:13; Zek 13:1; Yn 4:10,14; Ufu 21:6; Mdo 26:18; Efe 5:8; Kol 1:13; 1 Pet 2:9]
Katika nuru yako tutaona nuru.
10Uwadumishie wakujuao fadhili zako,[#Yer 22:16]
Na wanyofu wa moyo uaminifu wako.
11Mguu wa kiburi usinikaribie,
Wala mkono wa wasio haki usinifukuze.
12Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu;
Wameangushwa chini wasiweze kusimama.