Zab 41

Zab 41

Hakikisho la Msaada wa Mungu na Ombi la Uponyaji

1Heri amkumbukaye mnyonge;[#Mit 14:21; Mk 10:21]

BWANA atamwokoa siku ya taabu.

2BWANA atamlinda na kumhifadhi hai,

Naye atafanikiwa katika nchi;

Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.

3BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.

Katika ugonjwa wake umemtandikia.

4Nami nalisema, BWANA, unifadhili,[#Zab 6:2]

Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi.

5Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya,

Atakufa lini, jina lake likapotea?

6Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo,[#Zab 12:2]

Moyo wake hujikusanyia maovu,

Naye atokapo nje huyanena.

7Wote wanaonichukia wananinong’ona,

Wananiwazia mabaya.

8Neno la kisirani limemgandama,

Na iwapo amelala hatasimama tena.

9Msiri wangu tena niliyemtumaini,[#Mt 26:23; Oba 1:7; Mk 14:18; Lk 22:21; Yn 13:18]

Aliyekula chakula changu,

Ameniinulia kisigino chake.

10Lakini Wewe, BWANA, unifadhili,

Uniinue nipate kuwalipa.

11Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami,

Kwa kuwa adui yangu hasimangi kwa kunishinda.

12Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza,[#Zab 34:15; Mdo 2:28]

Umeniweka mbele za uso wako milele.

* * *

13Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli,[#Zab 106:48]

Tangu milele hata milele. Amina na Amina.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania