The chat will start when you send the first message.
1Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki,[#Zab 7:8]
Uniokoe na mtu wa hila asiye haki.
2Kwa kuwa Wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini umenitupa?[#Zab 28:7; Isa 26:4]
Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
3Niletewe nuru yako na kweli yako ziniongoze,[#Zab 2:6; 3:4]
Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata maskani yako.
4Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye
furaha yangu na shangwe yangu;
Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.
5Nafsi yangu, kwa nini kuinama,[#Zab 42:5,11]
Na kufadhaika ndani yangu?
Umtumaini Mungu;
Kwa maana nitakuja kumsifu,
Aliye afya ya uso wangu,
Na Mungu wangu.