The chat will start when you send the first message.
1Sikieni haya, enyi mataifa yote;
Sikilizeni, ninyi nyote mnaokaa duniani.
2Watu wakuu na watu wadogo wote pia,
Tajiri na maskini wote pamoja.
3Kinywa changu kitanena hekima,
Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara.
4Nitatega sikio langu nisikie mithali,[#Zab 78:2]
Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi
5Kwa nini niogope siku za uovu,
Ubaya ukinizunguka miguuni pangu?
6Wa hao wanaozitumainia mali zao,
Na kujisifia wingi wa utajiri wao;
7Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake,[#Mt 16:26]
Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake,
8(Maana fidia ya nafsi zao ina gharama,[#Ayu 36:18]
Wala hana budi kuiacha hata milele;)
9ili aishi sikuzote asilione kaburi.[#Ebr 9:27; Zab 89:48]
10Naam, ataliona, hata wenye hekima hufa;
Mpumbavu na mjinga hupotea pamoja,
Na kuwaachia wengine mali zao.
11Makaburi ni nyumba zao hata milele,
Maskani zao vizazi hata vizazi.
Hao waliotaja mashamba yao
Kwa majina yao wenyewe.
12Lakini mwanadamu hadumu katika heshima,
Bali amefanana na wanyama wapoteao.
13Hiyo ndiyo njia yao, ujinga wao,
Nao walioko baada yao huyaridhia maneno yao.
14Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu,[#Dan 7:22; Mal 4:3; Lk 22:30; 1 Kor 6:2; 2 Tim 2:12; Ufu 2:26]
Na mauti itawachunga;
Watu wanyofu watawamiliki asubuhi;
Umbo lao litachakaa, kao lao ni kuzimu.
15Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu,[#Hos 13:14]
Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha.
16Usiogope mtu atakapopata utajiri,
Na fahari ya nyumba yake itakapozidi.
17Maana atakapokufa hatachukua cho chote;
Utukufu wake hautashuka ukimfuata.
18Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai,
Na watu watakusifu ukijitendea mema,
19Atakwenda kwenye kizazi cha baba zake
Hawataona nuru hata milele.
20Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili,[#Mhu 3:19-21]
Amefanana na wanyama wapoteao.