The chat will start when you send the first message.
1Ee Mungu, unirehemu,[#Kol 2:14]
Sawasawa na fadhili zako.
Kiasi cha wingi wa rehema zako,
Uyafute makosa yangu.
2Unioshe kabisa na uovu wangu,[#Eze 36:25; Zek 13:1; 1 Kor 6:11; Ebr 9:14; 1 Yoh 1:7; Ufu 1:5]
Unitakase dhambi zangu.
3Maana nimejua mimi makosa yangu[#Zab 32:5]
Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
4Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,[#Rum 3:4; Lk 15:21; Mwa 39:9]
Na kufanya maovu mbele za macho yako.
Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo,
Na kuwa safi utoapo hukumu.
5Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu;[#Ayu 14:4; Yn 3:6; Rum 5:12]
Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
6Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni;
Nawe utanijulisha hekima kwa siri,
7Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi,
Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji
8Unifanye kusikia furaha na shangwe,
Mifupa uliyoiponda ifurahi.
9Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu;
Uzifute hatia zangu zote.
10Ee Mungu, uniumbie moyo safi,[#Mit 20:9; Yer 13:27; Eze 11:19; Mdo 15:9; Efe 2:10]
Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
11Usinitenge na uso wako,[#Mwa 4:14; Eze 36:27; Rum 8:9]
Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
12Unirudishie furaha ya wokovu wako;[#Rum 8:15; 2 Kor 3:17]
Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
13Nitawafundisha wakosaji njia zako,
Na wenye dhambi watarejea kwako.
14Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu,
Uniponye na damu za watu,
Na ulimi wangu utaiimba haki yako.
15Ee Bwana, uifumbue midomo yangu,
Na kinywa changu kitazinena sifa zako.
16Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa,
Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.
17Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika;
Moyo uliovunjika na kupondeka,
Ee Mungu, hutaudharau.
18Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako,
Uzijenge kuta za Yerusalemu.
19Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki,[#Mal 3:3]
Na sadaka za kuteketezwa, na kafara.
Ndipo watakapotoa ng’ombe
Juu ya madhabahu yako.