Zab 53

Zab 53

Kushutumiwa kwa Wasiomwamini Mungu

1Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;[#Rum 3:10-12; Zab 10:4]

Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza,

Hakuna atendaye mema.

2Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu,[#Zab 33:13; 2 Nya 15:2]

Aone kama yuko mtu mwenye akili,

Amtafutaye Mungu.

3Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja,[#Mhu 7:29]

Hakuna atendaye mema,

La! Hata mmoja.

4Je! Wafanyao maovu hawajui?[#Yer 4:22]

Walao watu wangu kama walavyo mkate,

Hawakumwita MUNGU.

5Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu,

Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru.

Umewatia aibu,

Kwa sababu MUNGU amewadharau.

6Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni!

MUNGU awarudishapo wafungwa wa watu wake;

Yakobo atashangilia,

Israeli atafurahi.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania