The chat will start when you send the first message.
1Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi,[#Isa 26:20]
Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe.
Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako,
Hata misiba hii itakapopita.
2Nitamwita MUNGU Aliye juu,[#Zab 138:8]
Mungu anitimiziaye mambo yangu.
3Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa,[#Zab 144:5; 40:11]
Atukanapo yule atakaye kunimeza.
Mungu atazipeleka
Fadhili zake na kweli yake
4Nafsi yangu i kati ya simba,[#Mit 30:14; Zab 64:3]
Nitastarehe kati yao waliowaka moto.
Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale,
Na ndimi zao ni upanga mkali.
5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,[#Zab 108:5]
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6Wameweka wavu ili kuninasa miguu;[#Zab 9:15]
Nafsi yangu imeinama;
Wamechimba shimo mbele yangu;
Wametumbukia ndani yake!
7Ee Mungu, moyo wangu u thabiti,[#Zab 108:1]
Moyo wangu u thabiti.
Nitaimba, nitaimba zaburi,
8Amka, utukufu wangu.[#Amu 5:12]
Amka, kinanda na kinubi,
Nitaamka alfajiri.
9Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu,
Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.
10Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,[#Zab 108:4]
Na uaminifu wako hata mawinguni.
11Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.