Zab 58

Zab 58

Sala ya Kutaka Kisasi

1Ni kweli, enyi wakuu, mnanena haki?

Enyi wanadamu, mnahukumu kwa adili?

2Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu;[#Zab 94:20]

Katika nchi mnapima udhalimu wa mikono yenu.

3Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao;[#Zab 51:5]

Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.

4Sumu yao, mfano wake ni sumu ya nyoka;[#Zab 140:4]

Mfano wao ni fira kiziwi azibaye sikio lake.

5Asiyeisikiliza sauti ya waganga,

Ijapo wanafanya uganga kwa ustadi.

6Ee Mungu, uyavunje meno yao vinywani mwao;[#Ayu 4:10]

Ee BWANA, uyavunje magego ya wana-simba.

7Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi;

Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu.

8Kama konokono ayeyukaye na kutoweka,

Kama mimba iliyoharibika, isiyoliona jua,

9Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba,[#Mit 10:25]

Ataipeperusha kama chamchela,

Iliyo mibichi na iliyo moto.

10Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi;[#Kum 32:42; Ayu 22:19; Zab 18:47; Mit 10:11; Ufu 18:20]

Ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki.

11Na mwanadamu atasema,[#Rum 2:6-11; Ayu 34:11; Mhu 5:8; Yer 32:19; Eze 7:27; Rum 14:12; Ufu 2:23]

Hakika iko thawabu yake mwenye haki.

Hakika yuko Mungu

Anayehukumu katika dunia.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania