The chat will start when you send the first message.
1Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu;
Unilinde uhai wangu na hofu ya adui.
2Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya,[#Zab 143:9]
Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;
3Waliounoa ulimi wao kama upanga,[#Zab 57:4]
Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,
4Wapate kumpiga mkamilifu faraghani,
Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.
5Walijifanya hodari katika jambo baya;
Hushauriana juu ya kutega mitego;
Husema, Ni nani atakayeiona?
6Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili;
Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao,
Na moyo wake, huwa siri kabisa.
7Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha,
Kwa mshale mara watapigwa.
8Ndivyo watakavyokwazwa,[#Mit 12:13]
Ulimi wao wenyewe ukishindana nao.
Wote wawaonao watatikisa kichwa.
9Na watu wote wataogopa,
Wataitangaza kazi ya Mungu,
Na kuyafahamu matendo yake.
10Mwenye haki atamfurahia BWANA na kumkimbilia,[#Zab 32:11; Flp 4:4]
Na wote wenye moyo wa adili watajisifu.