The chat will start when you send the first message.
1Ee Mungu, uniokoe,
Ee BWANA, unisaidie hima.
2Waaibike, wafedheheke,[#Zab 109:29]
Wanaoitafuta nafsi yangu.
Warudishwe nyuma, watahayarishwe,
Wapendezwao na shari yangu.
3Warudi nyuma, na iwe aibu yao,
Wanaosema, Ewe! Ewe!
4Washangilie, wakufurahie,[#Isa 61:10; Hab 3:17; Rum 5:2; Flp 3:1; 1 Pet 1:2-9]
Wote wakutafutao.
Waupendao wokovu wako
Waseme daima, Atukuzwe Mungu.
5Nami ni maskini na mhitaji,[#Zab 40:17; Amu 5:28; Zab 141:1; Ebr 10:37; Ufu 22:20]
Ee Mungu, unijilie kwa haraka.
Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu,
Ee BWANA, usikawie.